Acheni Ninyi Acheni Kabisa

Acheni Ninyi Acheni Kabisa
Alt TitleWateteni Wanyonge na Yatima
Performed bySt. Veronicah Kariakoo
AlbumWalinizunguka Kama Nyuki
CategoryTafakari
ComposerF. Mtegeta
Views3,462

Acheni Ninyi Acheni Kabisa Lyrics

ACHENI NINYI

 1. Acheni ninyi, acheni kabisa, acheni kuwapendelea waovu
  Wateteeni wanyonge na yatima, wapeni haki masikini na fukara
  Waokoeni wanyonge na maskini katika makucha ya wadhalimu

 2. Acheni kutoa hukumu, hukumu isiyo ya haki kwa wanyonge
  {Kwa kuwa (kwa kuwa) wanyonge na maskini ni wa Mungu
  Msiwakandamize wanyonge kwa kuwatetea waovu } * 2
 3. Lakini ninyi hamjui, aliyewapa mamlaka ni nani
  Ni yeye (ni yeye) anaye uchukia uovu
  Anayeuchukia uovu na kuwapenda maskini
 4. Maisha ya dunia ni mafupi sana ndugu kumbukeni
  Na ninyi (na ninyi) mtakufa kama wakuu wengine
  Kama walivyokufa na kuyaacha madaraka na mali