Ni Wewe Tu

Ni Wewe Tu
Alt TitleKanuni Moja na Lugha Moja
Performed bySt. Veronicah Kariakoo
AlbumWalinizunguka Kama Nyuki
CategoryHarusi
ComposerBernard Mukasa
Views8,253

Ni Wewe Tu Lyrics

 1. Kanuni moja na lugha moja kwako we
  Siku zote nitakupenda kweli ee
  Ya ulimwengu hayanibadilishi we
  Siku zote nitakupenda kweli ee (haya)

  Katika raha, (ni wewe) katika shida, tena ni wewe tu * 2
  Ni wewe tu, ni wewe tu (tena ) ni wewe tena ni wewe tu * 2

 2. Tumefinyangwa kwa tope moja sisi ee
  Ni pumzi moja imetutengeneza ee
 3. Ingawa ulimwengu mtamu sana ee
  Sitaujali kwani wewe ni zaidi
 4. Mapungufu yako nitayachukulia
  Na msamaha sitakawia kukupa
 5. Nitakupenda kama nilivyoagizwa
  Kama Kristu alivyolipenda kanisa
 6. Maisha yetu yakamtukuze Baba
  Yamuinue Mwana yampambe Roho
Recorded by * St. Veronicah Kariakoo * Mt. Yuda Thadei Mbeya * Kapotive Singers Bukoba