Kimeeleweka
Kimeeleweka | |
---|---|
Alt Title | Kilichomfanya Baba Amtoe Mwanawe |
Performed by | St. Kizito Makuburi |
Album | Yuko Galilaya |
Category | Pasaka (Easter) |
Composer | Bernard Mukasa |
Views | 9,528 |
Kimeeleweka Lyrics
Kilichomfanya Baba amtoe mwanawe wa pekee
Kilichomfanya mwana akubali kufa kifo cha aibu
Leo kimefafanuliwa, leo kimeeleweka
Leo kimefafanuliwa, kimeeleweka, kimeeleweka!- Alimuona mwanadamu, anaanguka kuzimu
Akaja kumuinua, akakibugia kifo
Akashuka nacho, kuzimu kisha, akakiacha huko - Alijua udanganyifu wa Ibilisi mzushi
Akaja kuuharibu na kufunua ukweli
Kuzigaragaza, hila za mwovu, na kumuaibisha - Alimpenda mwanadamu, akampenda upeo
Kajifanananisha naye bali hakutenda dhambi
Akamuinua kiumbe huyu kampandisha hadhi
// h i t i m i s h o //
Amevishinda vita vya imani, mshindi
Amevaa utukufu na enzi, Mwokozi
Aeh atangaza mlango wa mbingu, u wazi
Aeh na urithi wa utawala
Kafufuka kama alivyosema yesu,
Amefufuka, ameyashinda mauti
Kafufuka (kafufuka) kama alivyosema Yesu,
Amefufuka (kafufuka) ameyashinda mauti
Kaivunja milango yote ya kuzimu,
Ameivunja, ameyashinda mauti, kafufuka . . .
Kaonyesha ya kwamba inawezekana,
Ameonyesha ameyashinda mauti, kafufuka . . .
Kwa hiyo, tuimbe aleluya ni shangwe kuu,
Kwa hiyo, tuimbe aleluya kwani Bwana ameyashinda mauti
Kwa hiyo, tuimbe aleluya ni shangwe kuu,
Kwa hiyo, tuimbe aleluya kwani Bwana ameyashinda mauti
Ameyashinda mauti, ameyashinda mauti,
ame ame ame ame ameyashinda mauti