Wamegawanyika
Wamegawanyika | |
---|---|
Alt Title | Nikiiwazia wazia Kazi ya Mwenyezi |
Performed by | Kwaya ya Malkia wa Mitume Parokia ya Vincent Palloti Arusha |
Album | Dira |
Category | Tafakari |
Composer | E. A. Minja |
Views | 4,189 |
Wamegawanyika Lyrics
Nikiiwaziawazia kazi yake Mwenyezi lo
Na alivyomuumba huyu mwanadamu
Tazama inavyopendeza kazi yake Mwenyezi lo
Na wengine kwa jinsi wanavyojipanga
{ Lakini sasa wamegawanyika
Tazama leo wao si kitu kimoja } *2
Wengine wanatafuta upendo ili kuwajali wengine
Wengine wamefanana na yule simba mnyama mkali
Wengine watafutacho ni mali tena utu umepotea
Hakuna kiburi cha kumwaga damu ya watu wengine- Unapowatazama wa nje eeh eeh
Na kwa jinsi wanavyopendeza eeh eeh
Hata kwenye miondoko yao eeh eeh
Wewe mwenyewe utawapenda eeh eeh
Lakini katika nyoyo zao eeh eeh
Wako katika sura ya kazi eeh eeh
Kwa kweli katika roho zao eeh eeh
Upendo kwao ni kama chambo eeh eeh - Na wengine wanapojipamba eeh eeh
Utawadhania malaika eeh eeh
Nyumba magari ya kifahari eeh eeh
Mwendo wao ni wenye heshima eeh eeh
Tembea wataongea yao eeh eeh
Kwa upole upendo amani eeh eeh
Kumbe moyoni wana kikao eeh eeh
Leo iwe ni zamu ya nani eeh eeh - Wamezoea kupata mali eeh eeh
Bila kuwa na moyo wa utu eeh eeh
Kuwatoa wengine kafara eeh eeh
Si tatizo bora wafaulu eeh eeh
Kukata viungo vya wenzao eeh eeh
Kwao wanachojali ni mali eeh eeh
Na wengine kufanywa pepeta eeh eeh
Utu si kitu bora ni mali eeh eeh - Kweli wachuna ngozi wenzao eeh eeh
Sasa ni zamu ya albino eeh eeh
Tatizo la yote hayo ni mali eeh eeh
Pengine watabadili wazo eeh eeh
Na kusema sasa ni weupe eeh eeh
Kisha waseme sasa wafupi eeh eeh
Wataongeza sasa wanene eeh eeh
Wapate mali kishirikina eeh eeh