Ninajisikia Mzuri
| Ninajisikia Mzuri |
|---|
| Performed by | - |
| Album | Watikisa Kibuyu |
| Category | Tafakari |
| Composer | E. A. Minja |
| Views | 3,082 |
Ninajisikia Mzuri Lyrics
Ninajisikia mzuri (mimi) na mkamilifu
Ninajisikia mkweli (tena) nisiye na hila
Ninajisikia msafi (mimi) kwa matendo yangu
Ninajisikia ni mwema (tena) nisiye na dhambi
- Mbele ya watu najituma, kama mtu mwema
Matendo yangu polepole, ya unyenyekevu
Kumbe huu ni wasifu wangu, wasifu wa nje
Wa ndani mwenendo mbaya wenye sifa mbaya
- Kupenda mambo ya uwongo, tena ya uzushi
Daima nayasisitiza, ndiyo kazi yangu
Majirani wakigombana ninasikiliza,
Kumbe chanzo cha yote hayo, hii ni siri yangu
- Ninakitumia kioo, ninajing'arisha
Kana kwamba mwuumba wangu alinikosea
Kumbe kwa nje napendeza, kama malaika
Kwa ndani mimi ni shetani, mwenye pembe kali
- Hebu tazama moyo wako, ukaubadili
Kimatendo hata mawazo, uwe mtu mwema
Mwenendo mbaya daima unafananishwa
Na kumpepea shetani asichoke kwa kazi