Amka Ewe Usinziaye
Amka Ewe Usinziaye | |
---|---|
Performed by | - |
Album | Kila Kunapokucha |
Category | Tafakari |
Composer | Victor Aloyce Murishiwa |
Views | 3,960 |
Amka Ewe Usinziaye Lyrics
Amka ewe usinziaye, amka ewe usinziaye
Amka, amka, fungua macho, amka
Pesa ni kitu cha kushangaza
Imezitega nyoyo za watu tazama,
Tazama uaminifu hakuna
Imejenga matabaka kwa maskini na matajiri, pesa
Imekuwa ni kitanzi, inafilisha hata sheria, pesa
Inagombanisha ndugu kwa ndugu pesa (tena)
Imekuwa ndiyo mzizi wa tamaa
Lakini ajabu ni kwamba,
Pesa kamwe pesa kamwe,
haitanunua mbingu ee Mungu
kama matajiri wangemiliki hewa,
maskini wangekuwa wapi
Kama matajiri wangemiliki mbingu,
maskini wangekosa haki- Pesa ni rafiki kwenye shida zako
lakini pesa ni adui kwenye raha zako - Pesa yabadili msimamo wako
Tazama pesa ni mbolea hustawisha dhambi - Pesa ni mtego kwa imani yako
Na tena pesa ni kioo kwa tabia yako
Recorded also by St. Claire Gatimu Kawangware, Nairobi