Anameremeta

Anameremeta
Choir-
CategoryBikira Maria
ComposerF. F. Ngwila

Anameremeta Lyrics

Anameremeta sana, anameremeta kama lulu
Hakika ni nyota ya asubuhi
Huyu ndiye yule mama, mama yake Bwana Yesu Kristu
Hakika ni mama Mama wa Mungu

Kwa nini tusimshangilie, (tena) tukirukaruka kwa furaha(pia)
Na vigelegele tuvipige tukimshangilie mama Maria
Kwani kupitia kwake mama (huyo) ukombozi wetu umefika (kwetu)
Kwa nini tusimwite Yesu tukiegemea kwake Maria

 1. Mama huyu mama gani, mama mwenye moyo safi
  Mama aliyereta nuru ya kuangaza kote
  Mama anameremeta, tena anang'ara sana
  Anang'ara kama lulu, lulu ya thamani kubwa
 2. Watakatifu Mbinguni wanamsifu Maria
  Nao wanameremeta wakiitazama nuru
  Mama huyu ni wa nuru, ni nuru ya ulimwengu
  Tena anang'ara sana pia anaangaza
 3. Maria naye Yosefu, walokuwa naye Yesu
  Nao wanang'ara sana pia wanameremeta
  Nasi tunaomsifu kuwa Maria ni Mama
  Nasi tunang'ara sana pia tutameremeta