Angalia Jinsi Mkulima
Angalia Jinsi Mkulima | |
---|---|
Performed by | - |
Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
Composer | Perfect Marandu |
Views | 4,724 |
Angalia Jinsi Mkulima Lyrics
{Angalia jinsi mkulima anavyofurahi-ya,
Kuyachuna matunda (yale) yaliyoiva vizuri
Katika bustani yake }* 2
Na pia kuyatupa yale mabovu mbali
Na kuyaacha yaliyo mabichi ili yapate kuiva vizuri
ili aweze kuyachuma tena- Vivyo hivyo Mungu hufurahia kuwaita kwake wale walio safi
na kuwapa nafasi ya kutubu wale wenye dhambi - Ni wajibu kwangu mimi na wewe,kutubu kwani hakuna ajuaye siku
Wala saa ambayo Mungu Baba atamwita kwake - Ewe ndugu yangu unafikiria nini kuingia katika jubilei
Ya miaka elfu mbili ukiwa na mzigo wa dhambi - Yafaa nini mtu kupata raha zote za dunia ambazo ni zam muda
Na kutupwa katika moto ule wa milele yote - Mimi na wewe tutumie nafasi hii tuliyopewa tutubu dhambi zetu
Mtu asijeijutia siku atakayoitwa
Recorded also by St. Gabriel Biticha Kisii