Login | Register

Sauti za Kuimba

Angalia Jinsi Mkulima Lyrics

ANGALIA JINSI MKULIMA

@ Perfect Marandu

{Angalia jinsi mkulima anavyofurahi-ya,
Kuyachuna matunda (yale) yaliyoiva vizuri
Katika bustani yake }* 2
Na pia kuyatupa yale mabovu mbali
Na kuyaacha yaliyo mabichi ili yapate kuiva vizuri
ili aweze kuyachuma tena

 1. Vivyo hivyo Mungu hufurahia kuwaita kwake wale walio safi
  na kuwapa nafasi ya kutubu wale wenye dhambi
 2. Ni wajibu kwangu mimi na wewe,kutubu kwani hakuna ajuaye siku
  Wala saa ambayo Mungu Baba atamwita kwake
 3. Ewe ndugu yangu unafikiria nini kuingia katika jubilei
  Ya miaka elfu mbili ukiwa na mzigo wa dhambi
 4. Yafaa nini mtu kupata raha zote za dunia ambazo ni zam muda
  Na kutupwa katika moto ule wa milele yote
 5. Mimi na wewe tutumie nafasi hii tuliyopewa tutubu dhambi zetu
  Mtu asijeijutia siku atakayoitwa
Angalia Jinsi Mkulima
COMPOSERPerfect Marandu
CATEGORYKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
MUSIC KEYE Major
TIME SIGNATURE6
16
NOTES Open PDF


Recorded also by St. Gabriel Biticha Kisii
 • Comments