Asante Mungu Mwenyezi
| Asante Mungu Mwenyezi | |
|---|---|
| Performed by | St. Veronicah Kariakoo |
| Album | Walinizunguka Kama Nyuki |
| Category | Thanksgiving / Shukrani |
| Composer | Victor Aloyce Murishiwa |
| Views | 8,568 |
Asante Mungu Mwenyezi Lyrics
Asante Mungu Mwenyezi, asante (asante)
Muumba mbingu na nchi, asante
{ Nakushukuru Mungu wangu kwa mema yako yote (leo)
Milele hata milele nitaimba sifa zako (mimi)
Nitaimba sifa zako kwa shangwe } * 2- Kwa wingi wa fadhili zako nakushukuru Bwana
Kwa wingi wa rehema zako asante Mungu wangu - Umeniumba mimi Bwana ukanipa akili
Ninakushukuru ee Mungu kwa moyo wangu wote - Nitaziimba sifa zako katika kusanyiko
Nitatanganza Neno lako milele na milele