Bwana Amejaa Huruma
Bwana Amejaa Huruma |
---|
Performed by | - |
Category | TBA |
Composer | John Mgandu |
Views | 6,448 |
Bwana Amejaa Huruma Lyrics
BWANA AMEJAA HURUMA
Bwana amejaa huruma na neema
Haoni hasira upesi ni mwingi wa fadhili
Maana Mbingu zilivyoinuka juu ya nchi
Kadiri ile ile, rehema zake ni kuu kwa wamchao
- Ee nafsi yangu umhimidi Bwana
Na vyote vilivyo ndani yangu
Vilihimidi Jina lake Takatifu
Ee nafsi yangu umhimidi Bwana
Wala usizisahau fadhili zake zote
- Akusamehe maovu yako yote
Akuponya magonjwa yako yote
Aukomboa uhai wako na kaburi
Akutia taji la fadhili na rehema
Aushibisha neema uzee wako
- Bwana ndiye afanyaye mambo ya haki
Na hukumu kwa wote wanaoonewa
Alimjulisha Musa njia zake
na wana wa Israeli matendo yake
Wana wa Israeli matendo yake