Bwana Yesu Amenipigania
| Bwana Yesu Amenipigania |
|---|
| Performed by | Same KMJ |
| Album | Watikisa Kibuyu |
| Category | Zaburi |
| Composer | Augustine Rutta |
| Views | 6,407 |
Bwana Yesu Amenipigania Lyrics
Bwana Yesu amenipigania, dhidi ya jeshi la shetani lote
{ Farasi na wapanda farasi wake,
Amewatupa baharini na silaha zao wameangamia
Nami nitainuka leo, nikamshangilie jemedari mkuu Bwana wa vita } * 2
- Adui shetani alitamba akirandaranda popote
Sasa ametupwa baharini na jeshi lake lote
Hebu fikiri Bwana Yesu Getsemani na Kalvari
Alimshinda kwa msalaba na sisi tumekombolewa
- Ulipolala kwenye mauti alitufungulia mlango
Alitutoa kule kuzimu akatuweka pa salama
Msalaba wetu ndiyo kinga silaha nayo ngao yetu
Tukapigane kwa ujasiri tupate kuingia kwake