Bwana Alitutendea Mambo Makuu

Bwana Alitutendea Mambo Makuu
Performed bySt. Cecilia Mirerani
AlbumUpendo na Amani
CategoryZaburi
ComposerDeo Mhumbira
Views9,422

Bwana Alitutendea Mambo Makuu Lyrics

  1. Bwana alitutendea mambo makuu
    Bwana alitutendea mambo makuu
    tulikuwa tukifurahi tukifurahi
    (Tulikuwa tukifurahi) tulikuwa tukifurahi
    Alitutendea mambo makuu
    Bwana alitutendea mambo makuu
    Tulikuwa tukifurahi tukifurahi
    (Tulikuwa tukifurahi) tulikuwa tukifurahi

  2. Bwana alipowarejesha mateka wa sayuni
    Tulikuwa kama waotao ndoto
    Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko
    Na ulimi wetu kelele za shangwe
  3. Ndipo waliposema katikati ya mataifa
    Bwana amewatendea mambo makuu
    Bwana alitutendea mambo makuu
    Tulikuwa tukifurahi
  4. Bwana uwarejeshe watu wetu waliofungwa
    Kama vijito vya kusini
    Wale watu wapandao kwa machozi
    Watavuna kwa kelele za shangwe