Bwana Ndiye Mchungaji Wangu

Bwana Ndiye Mchungaji Wangu
Performed bySt. Maurus Kurasini
AlbumHubirini Kwa Kuimba
CategoryZaburi
ComposerJohn Mgandu
Views11,704

Bwana Ndiye Mchungaji Wangu Lyrics

  1. { [ s ] Bwana ndiye mchungaji wangu
    [ w ] Bwana ndiye mchungaji wangu
    Sitapungukiwa na kitu * 3 } * 2

  2. Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu
    Katika malisho ya majani mabichi hunila-za
    Kando ya maji ya utulivu hu-niongoza
  3. Huniuhuisha nafsi yangu, na kuniongoza
    Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake
    Nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya
  4. Huandaa meza mbele yangu, machoni pa watesi wangu
    Hunipaka mafuta kichwani kichwani mwangu
    Na kikombe kikombe changu ki-nafurika
  5. Kwa hakika wema na fadhili zitanifuata
    Siku zote za maisha yangu maisha yangu
    Nami nitakaa nyumbani mwa Bwa-na milele