Bwana ni Nuru Yangu

Bwana ni Nuru Yangu
Performed byKwaya ya Moyo Safi wa Bikira Maria, Unga Limited Arusha
AlbumNikupe Nini Mungu Wangu
CategoryZaburi
ComposerDeo Mhumbira
Views15,968

Bwana ni Nuru Yangu Lyrics

  1. { Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, nimwogope nani
    Bwana ni ngome ya uzima wangu, nimhofu nani } *2

  2. Watesi wangu na adui zangu, walijikwaa wakaanguka
    Jeshi lijapo kupigana nami, moyo wangu hautaogopa
  3. Vita vijaponitokea hata hapo nitatumaini
    Neno moja nalitaka kwa Bwana, nalo ndilo nitalitafura
  4. Nikae nyumbani mwa Bwana, siku zote za maisha yangu
    Niutazame uzuri wa Bwana na kutafakari hekaluni mwake