Bwana Moyo Wangu
| Bwana Moyo Wangu | |
|---|---|
| Performed by | Kwaya ya Moyo Safi wa Bikira Maria, Unga Limited Arusha |
| Album | Tufurahi |
| Category | Wito |
| Composer | H Makelele |
| Views | 30,684 |
Bwana Moyo Wangu Lyrics
{ Bwana moyo wangu hauna kiburi
Nayo macho yangu hayainuki } *2
{ Wala sijishughulishi na mambo makuu
Yanayozishinda nguvu zangu } *2- Hakika nimetuliza nafsi yangu, na pia kuinyamazisha
- Kama mtoto aliyeachishwa ziwa, kifuani kwa mamaye
- Ndivyo roho yangu ilivyo kwangu mimi, tangu leo hata milele