Ninakushukuru Bwana
Ninakushukuru Bwana |
---|
Alt Title | J. Mugangos |
Performed by | - |
Album | Haya Tazameni (Vol 21) |
Category | Thanksgiving / Shukrani |
Composer | J. Mugangos |
Views | 8,577 |
Ninakushukuru Bwana Lyrics
- Ninakushukuru Bwana, ninakushukuru Bwana
Kwa mema unayonijalia ninakushukuru
Ninakushukuru Bwana
mimi ninakushukuru Bwana mimi ninakushukuru Bwana
Ninakushukuru Bwana
mimi ninakushukuru Bwana mimi ninakushukuru Bwana
- Nina kila sababu ya kukushukuru Bwana
(Tena) Tena inanipasa nitoe shukrani zangu,
Kwako wewe Muumba wangu muumba wangu, ewe Mungu wangu
- {Ninatazama jinsi nilivyo mimi,
ni wewe Bwana uliyeniumba mimi (Bwana)
Ukanipa uzima, ukanipa uzima, pia na akili } * 2
- Na tazama na pia vitu vyote nilivyo navyo
Nimevipata kutoka kwako Bwana Mungu wangu
Kwa nini nisishukuru, kwa nini?
Kwa nini nisikushukuru Bwana
Kwa nini nisikushukuru Bwana
Kwa nini nisikushukuru Bwana Muumba wangu
(Yanipasa) Yanipasa nikushukuru
- { Ninakushukuru kwa moyo wangu wote
Ninakushukuru Mungu wangu
Ninakushukuru Mungu wangu
Ninakushukuru Mungu wangu kwa moyo wangu wote } * 2
- Ninakusihi ewe Bwana Mungu wangu
uzipokee shukrani zangu
Ingawaje shukrani zangu hazilingani na wema wako kwangu, ee Mungu wangu
- Ninafahamu Bwana unanipenda, ingawaje
Waujua udhaifu wangu na mawazo yangu yote ya kila siku
Na maneno na matendo yangu yote
- Ninajiuliza nikushukuru jinsi gani Mungu wangu
Nitakuimbia wimbo wa sifa
Wimbo ule ulio bora wimbo wa shukrani, wa shukrani
Niyatangaze matendo yako makuu
Na sifa zako na wema wako wakati wote
Na pia mahali pote
- Nitalitangaza Neno lako kwa watu wote, wakuheshimu wakufuate wewe
Ninakuomba uniimarishe pia unilinde, ili nikufuate wewe daima na daima
nami nitakushukuru siku zote za maisha yangu nisadie Bwana
- Ninakushukuru Bwana, ninakushukuru Bwana
Kwa mema unayonijalia ninakushukuru
Ninakushukuru Bwana, ninakushukuru Bwana
Kwa mema unayonijalia ninakushukuru
- Ninatoa asante kwako Bwana Mungu wangu
Asante, asante, asante,
Ninatoa asante kwako Bwana Mungu wangu
Asante, asante, asante,
- a-asante (asante), a-asante (asante) , a-asante (asante asante),
asante asante asante (asante)
- a-asante (asante), a-asante (asante) , a-asante (asante asante),
asante Mungu Baba asante