Tuidhihirishe Imani
| Tuidhihirishe Imani |
|---|
| Alt Title | Waamini Tunaalikwa |
| Performed by | - |
| Category | Faith |
| Composer | Charles Saasita |
| Views | 3,335 |
Tuidhihirishe Imani Lyrics
Waamini tunaalikwa, kuidhihirisha imani yetu kwa matendo
{Ni mwaliko wa Baba Mtakatifu, ni mwaliko wa Kanisa
Kuipa uhai imani tunayoikiri,
imani tunayoiadhimisha, imani tunayoiishi } * 2
- Imani tunayoikiri,
Ndiyo kusadiki kwa Mungu mmoja mwumba Mbingu na nchi
Ndiyo kusadiki kwa Bwana mmoja Yesu Kristu
Ndiyo kusadiki kwa Roho Mtakatifu
- Imani tunayoikiri,
Ndiyo kusadiki kwa kanisa moja takatifu Katoliki la mitume
Kuungama ubatizo mmoja, ufufuko wa wafu na uzima wa milele
- Imani tunayoadhimisha, ndiyo sakramenti za kanisa
Zilizo chemichemi za neema tupatazo kwa Mungu
Sisi tunaomwamini Kristu na kumfuata
- Imani tunayoiishi, ndiyo kuziweka maishani mwetu amri zote za Mungu
Bila kuyumbishwa na hisia za uhuru wa kidunia
Na kubaki katika mtazamo wa Kimungu kwa mafundisho ya kanisa