Ee Bwana Ninakuja
Ee Bwana Ninakuja Lyrics
Ee Bwana ninakuja mbele ya altare yako
Unipokee Bwana wangu nikutumikie
Ninajitolea kwako maisha yangu yote
Nakuomba unitakase niwe mtumishi wako
Hayana haja ya dunia nikutumikie wewe
Unijaze roho wako niwe mtumishi mwaminifu
- Ninakuja kwako Bwana, unipokee Muumba wangu
Nahitaji wito ewe Bwana Mungu wangu
Unijaze roho wako nikutumikie
- Bila msaada wako, peke yangu hakika siwezi
Nahitaji nguvu yako Bwana inisaidie
Unijaze roho wako nikutumikie
- Ni vikwazo vingi sana, vya shetani vinavyonisonga
Nahitaji neema yako ili nivishinde vyote
Unijaze roho wako nikutumikie