Akawaonyesha Mana

Akawaonyesha Mana
ChoirSt. Cecilia Namanga
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerE. Pastory

Akawaonyesha Mana Lyrics

{Akawaonyesha mana ili wale,
akawapa nafaka ya mbinguni
Mwanadamu akala chakula cha mashujaa
Aliwapelekea chakula cha kuwashibisha} * 2

 1. Mambo tuliyoyasikia na kuyafahamu
  Ambayo mababa zetu walituambia
 2. Lakini aliamuru mawingu ya mbingu
  Akaifungua milango ya mbinguni
  Akawanyeshea mana ili wale
  Akawapa nafaka ya Mbinguni
 3. Mwanadamu akala chakula cha mashujaa
  Aliwapelekea chakula kuwashibisha
  Aliwapeleka kwa mlima wake takatifu
  Mlima alioununua kwa mkono wake wa kuume