Nyumba ya Roho
| Nyumba ya Roho |
|---|
| Alt Title | Mungu wangu Nikujue Vipi |
| Performed by | - |
| Album | Nyumba ya Roho |
| Category | TBA |
| Composer | Charles Ruta |
| Views | 3,713 |
Nyumba ya Roho Lyrics
NYUMBA YA ROHO
Mungu wangu nikujue mimi, Mungu wangu nikupende
Mungu nikutumikie, kisha niurithi ufalme Mbinguni * 2
(wewe) roho umenipa ee, (kisha) ukaihifadhi vizuri
(yaani) ndani ya mwili ee (kwani) mwili ni nyumba ya rho
- Ndiwe mungu peke yako, wa kuabudiwa ni wewe
Nishike kitakatifu siku hiyo siku yako
nisilitaje kabisa bure jina lako Mwenyezi
Ulimi wa mwili wangu usiiponze roho yangu
- Niwaheshimu wazazi, ili nisiwasononeshe
Uhai wa binadamu niuthamini yani nisiuue
Kuiba nijiepushe, kusema uwongo niache
Mwili wangu usizini ndipo roho yangu itapona
- Niepuke kutamani yote yasiyo mali yangu
Naye mwanamke asiye mke wangu yani sio wangu
Hapo ndipo nitakuwa nimeutumia vizuri
Mwili ulioiumbia roho ifike Mbinguni juu