Ni Mpango wa Mungu
| Ni Mpango wa Mungu |
|---|
| Performed by | - |
| Album | Milele Milele Nitakusifu |
| Category | Tafakari |
| Views | 5,136 |
Ni Mpango wa Mungu Lyrics
{Ni mpango wa Mungu Baba, kuniumba hivi nilivyo
Na jinsi alivyoniumba, ili yeye atukuzwe } * 2
- Tazama mimi ni kipofu, nawe mwenzangu unaona
Ni mpango wa Mungu Baba ili kwa hilo atukuzwe
- Tazama mimi ni kiwete, nawe mwenzangu watembea
Ni mpango wa Mungu Baba ili kwa hilo atukuzwe
- Tazama mimi ni mweusi, nawe mwenzangu ni mweupe -
Tazama mimi ni mfupi, nawe mwenzangu ni mrefu -
- Tazama mimi maskini, nawe mwenzangu ni tajiri -
Tazama unao watoto, bali mimi nawatafuta -