Ufalme wa Mbinguni

Ufalme wa Mbinguni
Performed by-
CategoryMafundisho ya Yesu
ComposerJoseph Makoye
Views5,973

Ufalme wa Mbinguni Lyrics

  • Ufalme wa Mbinguni umefanana na mtu
    aliyepanda mbegu njema katika konde lake
    Lakini watu walipolala akaja adui yake
    Akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake
  • Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa
    yakaonekana na magugu
    Watumwa wa mwenye nyumba wakamwambia
    Bwana hukupanda mbegu njema katika konde lako
    Limepata wapi basi magugu
  • Akawaambia,
    Adui ndiye aliyetenda hivi
    Watumwa wakasema,
    Basi wataka twende tukayakusanye
    Naye akasema,
    Na msije mkakusanya magugu, na kuzitwaa ngano pamoja nayo
  • Viacheni vyote vikue mpaka wakati wa mavuno
    Na wakati wa mavuno, nitawambia wavunao
    Yakusanye kwanza magugu, myafunge machicha machicha,
    mkayachome
    Bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu