Mwimbieni Bwana Wimbo

Mwimbieni Bwana Wimbo
Performed byKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
AlbumKwa Wingi wa Fadhili
CategoryZaburi
Views11,161

Mwimbieni Bwana Wimbo Lyrics

  1. {Mwimbieni Bwana wimbo mpya kwa maana ametenda (ametenda)
    Kwa maana ametenda (ametenda) ametenda mambo ya ajabu
    Ametenda mambo ya ajabu, ametenda mambo ya ajabu } * 2

  2. Mkono wa kuume wake mwenyewe, mkono wake mtakatifu
    umemtendea wokovu, umemtendea wokovu, umemtendea wokovu
  3. Bwana ameufunua wokovu machoni pa mataifa yote
    Ameyadhihirisha haki, kadhihirisha haki yake, kadhihirisha haki yake
  4. Amezikumbuka rehema zake na uaminifu wake wote
    Katika nyumba ya wana wana wake wa Israeli, wana wake wa Israeli
  5. Mshangilieni Bwana nchi yote inueni sauti zenu
    Imbeni kwa furaha kubwa, imbeni imbeni zaburi, imbeni imbeni zaburi