Tunu Yetu
   
    
     
        | Tunu Yetu | 
|---|
| Alt Title | Utulivu na Amani | 
| Performed by | - | 
| Album | Milele Milele Nitakusifu | 
| Category | Tafakari | 
| Views | 2,991 | 
Tunu Yetu Lyrics
 
             
            
- Pema huwa pema hujapopema, ukishapema si pema tena
 Edeni ilikuwa haki yetu, tukaasi tukatupwa pipani
 Utulivu na amani Tanzania ni silaha,
 tudumishe amani yetu tunu yetu -
 Utulivu na amani Tanzania ni silaha,
 tudumishe amani yetu tunu yetu jema
- Tumepewa kwa upendeleo, utulivu Tanzania ni tunu
 Hatukuinunua kwa fedha, amani ni namba moja (amani)
- Madaraka yasitudanganye, utulivu Tanzania ni tunu
 Utajiri usituchanganye, amani ni namba moja (amani)
- Tunapokosoana wapendwa, utulivu Tanzania ni tunu
 Tunapoelezana ukweli, amani ni namba moja (amani)
- Kwenye shibe na kwenye furaha, utulivu Tanzania ni tunu
 Kwenye njaa na kwenye huzuni, amani ni namba moja (amani)
- Tukumbuke ametupa bure, utulivu Tanzania ni tunu
 Tukimwuzi ataiondoa, amani ni namba moja (amani)
 
 Tuitunze kama yai, tunu yetu jema
 Tuilee na tuipambe, tunu yetu jema
 Tuitunze itutunze, tunu yetu jema
 Tuilishe na tuinyweshe, tunu yetu jema
 
 Tunu yetu jema, tunu yetu jema
 Tunu yetu jema ee, tunu yetu jema
 Tuitunze siku zote, tunu yetu jema