Hii ni Sauti
Hii ni Sauti | |
---|---|
Performed by | Kwaya ya Moyo Safi wa Bikira Maria, Unga Limited Arusha |
Album | Milele Milele Nitakusifu |
Category | Majilio (Advent) |
Composer | E. F. Jissu |
Views | 6,085 |
Hii ni Sauti Lyrics
Hii ni sauti ya mtu yule, aliaye kutoka nyikani * 2
Itengezeni njia ya Bwana,yanyoosheni mapito yake * 2
Na wote wenye mwili watauona, wokovu wa Mungu aleluya * 2- Haya ng'oeni magugu yote, tusafishe tusafishe
Haya ng'oeni na mizizi yake, tusafishe tusafishe
{Tusaishe bila ya kinyongo, ndugu zangu tusafishe
Tusafishe kwa moyo mmoja, ndugu zangu tusafishe} - Tuichimbeni mizizi ya rushwa, tusafishe tusafishe
Tuyafukieni mashimo ya rushwa, tusafishe tusafishe
Tusafishe bila ya kinyongo, ndugu zangu tusafishe
Tusafishe kwa moyo mmoja, ndugu zangu tusafishe - Tujaze kifusi penye ubinafsi, tusafishe tusafishe
Tujenge upendo kwa jamii yote, tusafishe tusafishe
Tusafishe bila ya kinyongo, ndugu zangu tusafishe
Tusafishe kwa moyo mmoja, ndugu zangu tusafishe - Penye fitina tumwage Molami, tusafishe tusafishe
Penye majungu tumwage Molami, tusafishe tusafishe
Tusafishe bila ya kinyongo, ndugu zangu tusafishe
Tusafishe kwa moyo mmoja, ndugu zangu tusafishe - Tuzisafisheni nyumba za wachawi, tusafishe tusafishe
Tuzisafisheni kwa jina la Mungu, tusafishe tusafishe
(ii) Tusafisheni kwa imani, ndugu zangu tusafishe
Tusafishe siku ile yaja, ndugu zangu tusafishe - Tuing'oeni mizizi ya vita, tusafishe tusafishe
Tupalilie shamba la upedo, tusafishe tusafishe
(ii) Sisi sote ni watoto wa Mungu, ndugu zangu tupendane,
Sisi sote baba yetu mmoja, ndugu zangu tupendane.