Moyo Wangu na Utulie
Moyo Wangu na Utulie | |
---|---|
Performed by | St. Monica Lower Kabete Campus UoN |
Album | Uwe Nami Bwana |
Category | Tafakari |
Composer | JohnBosco Hosea |
Views | 4,873 |
Moyo Wangu na Utulie Lyrics
Moyo wangu na utulie kwako Bwana Mungu wangu - na mwokozi wangu
Maana wewe Bwana ndiwe kimbilio langu - tena mlinzi wangu *2
Wewe ndiwe Bwana - wa neema
Fadhili zako - ni za milele
Nikupe nini - Bwana mimi nikushukuru
Umenipa Bwana - na uhai
Pia na nguvu - za kutembea
Nafsi na roho - zangu kweli zimeridhika x2- Asubuhi niamkapo nitalisifu jina lako,
Kwa nyimbo nzuri za furaha mchana mimi nitaimba,
Usiku utimiapo, mimi nitakushukuru,
Kwa maana ninaishi kwa neema zako. - Kila nitembeapo mimi naona utukufu wako,
Wewe waniongoza mimi, kila hatua nipigayo,
Wewe ni Mungu mkuu, na mwenye Baraka tele,
Ninazo sababu tele za kukusifu wewe. - Ewe Bwana unanijua hata ndani ya moyo yangu,
Unaziona siri zangu hata wajua nitakalo,
Ninakuomba ee Bwana, uyajibu maombi yangu,
Kwa kuwa wewe ndiwe tumaini langu - Moyo wangu hukutafuta mchana hata na usiku,
Na mimi ninapokuita kweli wewe huniitika,
Karibu uishi kwangu, nami niwe ndani yako
Usikubali Bwana nitangane na wewe