Moyo Wangu na Utulie Lyrics

MOYO WANGU NA UTULIE

@ JohnBosco Hosea

Moyo wangu na utulie kwako Bwana Mungu wangu - na mwokozi wangu
Maana wewe Bwana ndiwe kimbilio langu - tena mlinzi wangu *2

Wewe ndiwe Bwana - wa neema
Fadhili zako - ni za milele
Nikupe nini - Bwana mimi nikushukuru
Umenipa Bwana - na uhai
Pia na nguvu - za kutembea
Nafsi na roho - zangu kweli zimeridhika x2

 1. Asubuhi niamkapo nitalisifu jina lako,
  Kwa nyimbo nzuri za furaha mchana mimi nitaimba,
  Usiku utimiapo, mimi nitakushukuru,
  Kwa maana ninaishi kwa neema zako.
 2. Kila nitembeapo mimi naona utukufu wako,
  Wewe waniongoza mimi, kila hatua nipigayo,
  Wewe ni Mungu mkuu, na mwenye Baraka tele,
  Ninazo sababu tele za kukusifu wewe.
 3. Ewe Bwana unanijua hata ndani ya moyo yangu,
  Unaziona siri zangu hata wajua nitakalo,
  Ninakuomba ee Bwana, uyajibu maombi yangu,
  Kwa kuwa wewe ndiwe tumaini langu
 4. Moyo wangu hukutafuta mchana hata na usiku,
  Na mimi ninapokuita kweli wewe huniitika,
  Karibu uishi kwangu, nami niwe ndani yako
  Usikubali Bwana nitangane na wewe
Moyo Wangu na Utulie
COMPOSERJohnBosco Hosea
CHOIRSt. Monica Lower Kabete Campus UoN
ALBUMUwe Nami Bwana
CATEGORYTafakari
 • Comments