Uwe Nami Bwana
Uwe Nami Bwana |
---|
Alt Title | Ninakushukuru Ee Mungu |
Performed by | - |
Album | Uwe Nami Bwana |
Category | Ekaristia (Eucharist) |
Composer | JohnBosco Hosea |
Views | 5,531 |
Uwe Nami Bwana Lyrics
- Ninakushukuru ee Mungu Baba
na kukusifu ewe mfalme wangu
Kwa sauti kuu tamu na za furaha
nacheza kwa madaha mbele yako Bwana
Nakushukuru kwa mema yote uliyonitendea mimi maishani mwangu.
Nakukaribisha (mimi) uwe nami Bwana (Yesu)
Uishi na mimi, Bwana daima milele.
Wewe Mungu mwema (kweli) na mwenye fadhili (nyingi)
Umenikubali japo mimi mwenye dhambi.
(Nakushukuru kwa kuniita kwako
Niwe mmoja wako daima milele x2)
- Umenipa mwili wako ee Bwana
chakula chenye uzima wa milele
Kikombe cha damu yako nimekunywa
kinywaji safi kinachonitakasa
Sitaona njaa wala kiu mimi maana u ndani ya roho yangu
- Nafsi yangu yakutafuta Bwana
kama ayala aonavyo kiu ya maji
Usiende mbali na mimi Bwana
maana ndiwe ngao ya maisha yangu
Na nguzo ya uhai wangu, tena wewe Bwana ndiwe tegemeo langu
- Ee Bwana unaijua nafsi yangu
na siri zote zilizo moyoni mwangu
Umezitakasa doa zangu zote
mimi ni kiumbe kipya mbele yako
Najitoa mimi kwako Bwana unitumie jinsi utakavyo wewe