Uwe Nami Bwana Lyrics

UWE NAMI BWANA

@ JohnBosco Hosea

 1. Ninakushukuru ee Mungu Baba
  na kukusifu ewe mfalme wangu
  Kwa sauti kuu tamu na za furaha
  nacheza kwa madaha mbele yako Bwana
  Nakushukuru kwa mema yote uliyonitendea mimi maishani mwangu.

  Nakukaribisha (mimi) uwe nami Bwana (Yesu)
  Uishi na mimi, Bwana daima milele.
  Wewe Mungu mwema (kweli) na mwenye fadhili (nyingi)
  Umenikubali japo mimi mwenye dhambi.
  (Nakushukuru kwa kuniita kwako
  Niwe mmoja wako daima milele x2)

 2. Umenipa mwili wako ee Bwana
  chakula chenye uzima wa milele
  Kikombe cha damu yako nimekunywa
  kinywaji safi kinachonitakasa
  Sitaona njaa wala kiu mimi maana u ndani ya roho yangu
 3. Nafsi yangu yakutafuta Bwana
  kama ayala aonavyo kiu ya maji
  Usiende mbali na mimi Bwana
  maana ndiwe ngao ya maisha yangu
  Na nguzo ya uhai wangu, tena wewe Bwana ndiwe tegemeo langu
 4. Ee Bwana unaijua nafsi yangu
  na siri zote zilizo moyoni mwangu
  Umezitakasa doa zangu zote
  mimi ni kiumbe kipya mbele yako
  Najitoa mimi kwako Bwana unitumie jinsi utakavyo wewe
Uwe Nami Bwana
ALT TITLENinakushukuru Ee Mungu
COMPOSERJohnBosco Hosea
ALBUMUwe Nami Bwana
CATEGORYEkaristia (Eucharist)
 • Comments