Mbinguni ni Furaha
Mbinguni ni Furaha |
---|
Performed by | - |
Album | Uwe Nami Bwana |
Category | Tafakari |
Composer | JohnBosco Hosea |
Views | 6,453 |
Mbinguni ni Furaha Lyrics
- Nimeahidiwa utukufu mbinguni – Kwake Mungu Baba
Nikamilishapo kazi yake Bwana – Aliyeniumba
Nitatunukiwa tuzo za kifalme – nikiwa mshindi
{t/b} Mbinguni ni furaha
Tutaimba, na kucheza
Tutaruka kwa furaha tukimwona Mungu,
Tuendapo paradiso aliyotuandalia sisi wateule x2
- Nyimbo za ushindi mimi nitaimba – Nikimwona Mungu
Sauti za mbinguni mimi nitapewa – naye Mungu wangu
Nikiwa na kwaya tamu za malaika – wote wa mbinguni
Tutaimba hosanna
- Makao ya kifahari mimi nitapewa – nilioandaliwa
Yaliyo na urembo usio na mifano – ya dhamani kubwa
Mandhari ya dhahabu na pia almasi – yanayometemeta
Mbinguni kwapendeza.
- Nitashangilia nikiwa barazani – pamoja na Mungu
Na watakatifu wake Mungu Baba – walionitangulia
Karamu ya wateule tutaandaliwa – kufutwa machozi,
Kwa shangwe na nderemo.
- Makao ya kifahari kweli ni mazuri – tena matulivu,
Yasiyo na njaa shida wala kifo – furaha kila siku,
Kazi ni kumsifu na kutukuza Mungu – milele amina
Huko ndiko nyumbani.