Wakenya Tuna Furaha

Wakenya Tuna Furaha
Performed by-
AlbumUwe Nami Bwana
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerJohnBosco Hosea
Views2,856

Wakenya Tuna Furaha Lyrics

  1. Wakenya tunafuraha (tele)
    Mungu kweli katubariki, nusu karne tuko imara.
    Njooni tufanye shangwe,
    Kwa vifijo na nderemo kuu, jubilee sherehe kubwa x2


    (Hakika) Miaka hamsini tuna uhuru,
    Tumeishi tukipendana
    Kwa umoja pia amani,
    Ni Baraka kuwa Mkenya x2
  2. Makabila ya Kenya (Yote)
    Yamerembesha nchi yetu, kwa nakshi za utamaduni.
    Lugha zinazovutia (sana)
    Zifurahishazo mioyo, na bado tunaelewana x2
  3. Madhari yapendezayo (sana)
    Milima mito na mabonde, nyufa mbuga na fuo za bahari.
    Maziwa yapendezayo (pia)
    Hifadhi za kihistoria, utalii tumeimarika x2
  4. Ulinzi tuko kijeshi (ona)
    Angani tuko imara, nchi maji usituchezee.
    Majasusi wale wabaya (na)
    Polisi tunao wa kutosha, kweli Kenya ni nchi salama x2.
  5. Viongozi waliosoma (pia)
    Sarakasi wanazielewa, walimwengu tunawatishia.
    Kuwa Mkenya ni Baraka (kweli)
    Tujenge nchi kwa furaha, Kenya yetu ni mimi na wewe x2