Mtakatifu Monica

Mtakatifu Monica
Performed by-
AlbumUwe Nami Bwana
CategoryWatakatifu
ComposerJohnBosco Hosea
Views10,496

Mtakatifu Monica Lyrics

  1. Ee mama mtakatifu Monica ewe mlinzi wetu (wanao)
    Wewe ndiwe mwangaza wetu ewe malkia.

    Sisi wote twakusalimu (ee mama)
    Na kukupa zote heshima, kwa kuwa nasi wanao katika imani x2)

  2. Kila tunapokulilia wewe kweli husikia sauti yetu mama
    Hutuliza mioyo yetu na nafsi zetu hupata amani.
  3. Ulikuwa mfano bora kwa wote walio na matatizo ya kijamii
    Ukaonyesha maombi na uvumilivu huleta umoja
  4. Kwa maisha yako ya ukinaifu wakristu wote tupate mafunzo bora,
    Tuishi tukigawana Baraka tupatazo zote kwa furaha.
  5. Sisi wana wa hii juia yako tunakuomba malkia utuongoze,
    Tuishi katika umoja, amani na upendo kutoka kwa Mungu.