Ee Mungu Nitakutafuta Mapema
Ee Mungu Nitakutafuta Mapema | |
---|---|
Performed by | St. Monica Lower Kabete Campus UoN |
Album | Uwe Nami Bwana |
Category | Zaburi |
Composer | JohnBosco Hosea |
Views | 8,157 |
Ee Mungu Nitakutafuta Mapema Lyrics
- [ t ] Ee Mungu, mungu wangu ee Bwana
[ w ] Nitakutafuta mapema, nafsi yakuonea kiu x2
[ t ] Maana
[ w ] Maneno yako ni Roho na uzima
Wewe unayo maneno ya uzima wa milee x2 - [ s ] Ee Mungu, Mungu wangu, nitakutafuta mapema,
Nafsi yakuonea kiu, mwili wakuonea shauku,
Kwenye nchi kavu yenye uchovu,
Nchi kavu isiyo na maji. - [ t ] Ndipo nilikutazama, katika patakatifu,
Nizione nguvu zako, na utukufu wako,
Maana fadhili zako, ni njema kuliko uhai,
Nafsi yangu itakusifu. - [ a ] Ndipo nitakubariki, wakati mimi naishi,
Nikiinua mikono yangu, nitaliomba jina lako,
Kwa utajiri wa karamu, nafsi yangu imeridhika,
Kwa midomo ya kinywa changu, nitakusifu wewe. - [ b ] Wewe ni msaada wangu,
Katika uvuli wa mbawa zako, hupiga kelele kwa furaha.
Nafsi yangu hushikamana, haraka kwako Bwana,
Kwa midomo ya kinywa cha-a-ngu, nitaku-usifu wewe.