Natamani Kuruka

Natamani Kuruka
Alt TitleNipishe Njia
Performed by-
CategoryEntrance / Mwanzo
ComposerBernard Mukasa
Views33,958

Natamani Kuruka Lyrics

  1. Nipishe njia nipeni nafasi
    Nimuonyeshe Mungu nilivyofurahi
    Nitamwimbia ngoma nitacheza
    Nimuonyeshe Mungu nilivyofurahi

    Natamani kuruka, nifika kule
    Nimuinue Mungu kwa mikono yangu
    Nimueleze kwa kinywa, changu mwenyewe
    Kwamba nimefurahi kwa upendo wake
    Bwana nashukuru, nashukuru nashukuru tu
    Ninashukuru kwa kunipenda bila mwisho
    Sina cha kusema, cha kusema cha kusema tu
    Ninashukuru kwa kunipenda bila mwisho

  2. Kaniinua kutoka shimoni -
    Akaniweka juu ya kinara -
    Nitazunguka kwa maringo tele -
    Na tabasamu lisilo kauka -
  3. Nitawashika wenzangu mikono -
    Tujiinue juu kwa pamoja -
    Wenzangu si mmejionea wenyewe -
    Mungu alivyo mwema wa ajabu -
  4. Nitaandika utukufu wake -
    Na wajukuu wangu wausome -