Msisumbuke Basi

Msisumbuke Basi
Performed byMaria Mt Mama wa Mungu Musoma
AlbumSilegei
CategoryMafundisho ya Yesu
ComposerMarcus Mtinga
Views2,883

Msisumbuke Basi Lyrics

  1. Msisumbuke, msisumbuke basi mkisema tule nini au tunywe nini au tuvae nini
    Kwa sababu hayo yo-te mataifa huyatafuta-
    Kwa sababu Baba yenu wa Mbinguni anajua kuwa mwayahitaji ha-yo yote
    {Bali utafuteni kwanza, ufalme wake,
    Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake
    Na ha-yo yote, na ha-yo yote mtazi-dishiwa mtazidishiwa } *2

  2. Ni yu-pi kwenu ambaye akijisumbua,
    Aweza kujiongeza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja
    Basi ikiwa hamuwezi neno lililo dogo,
    Kwa nini kujisumbua kujisumbua kwa ajili ya-yale mengine
  3. Yatafakarini maua jinsi yameavyo,
    hayatendi kazi hayatendi kazi hayatendi wa-la hayasokoti
    nami nawaambieni hata Suleiman katika fahari yake yote
    Hakuvikwa hakuvikwa vizuri kama moja wapo ya hayo
  4. Basi ikiwa Mungu huvika hivi majani ya kondeni
    Yaliyopo leo yaliyopo leo na kesho hutupwa karibuni karibuni
    Je hatawatendea nyinyi zaidi
    Enyi wa imani haba imani haba enyi wa imani haba