Ninataka Kuingia
Ninataka Kuingia | |
---|---|
Performed by | - |
Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
Views | 25,549 |
Ninataka Kuingia Lyrics
- Ninataka kuingia, mjini mwa Mungu
Nitashinda nitakaza mwendo nifike
Nikishikwa na shida, nikichoka njiani
Yesu unaniambia uningojee - Naitwa na Yesu Kristu enzini mwake
Nakimbia kukawia hakuna faida
Wote wachelewao hawatapata taji
Mimi sitaki kingine ila uzima - Elekeza macho yangu mlangoni pako
Niongoze nipe nguvu nikilemewa
Ninapojaribiwa, ninaposingiziwa
Yesu unisaidie nisikuache - Mkono wako unishike nisianguke
Najiona kuwa mnyonge nguvu i kwako
Neno lako ee Yesu linanipa uzima
Nikifika nitaimba umeniponya
* nikilemewa - some versions sing "ninapochoka"