Ewe Yesu Utufanye

Ewe Yesu Utufanye
Performed by-
CategoryInjili na Miito (Gospel)
Views2,988

Ewe Yesu Utufanye Lyrics

  1. Ewe Yesu utufanye watume wako,
    Tupe nguvu na ujasiri tueneze injili yako
    Tuwezeshe kudumisha mapenzi yako
    Na kufuata amri zote zitokazo kwako

  2. Ewe Bwana tuangazie (mwanga wako) *2
    Tu vipofu wa neno lako tuonyeshe njia yako
  3. Na imani tuongezee (tuwe huru) *2
    Kwani kamwe si watumwa, Yesu ametukomboa.
  4. Tujalie upendo wako (tupendane) *2
    Tuwapende watu wote kwani tu watoto wako.
  5. Mtume Paulo *2 mwalimu wetu, tuombee
    Ili tusitenganishwe (ili tuwe) na upendo wake Kristu
  6. Mtakatifu Cecilia (tuombee) Ili tusitenganishwe
    Na upendo wake Kristu, tuongoze njiani *3