Amini Kuna Chakula
   
    
     
         
          
            Amini Kuna Chakula Lyrics
 
             
            
- Amin, amin, nawaambieni kuna chakula kinachowafaa,
 Nacho chakula ndicho kile cha uzima wa milele
- Amin kweli, nawaambieni mwanitafuta.
 Si kwa sababu mlikula ule mkate.
 Si kwa sababu mliziona zile Ishara.
 Bali sababu mlikula mkashiba *2
- Msikitendee kazi chakula kinachopita.
 Bali, chakula kidumucho milele.
 Chakula Musa alichowapa hakiwafai,
 Kweli Babangu anawapa kifaacho
- Kile chakula chenye uzima kweli ni mimi
 Ajaye kwangu hataona njaa kamwe.
 Anayekula huu mwili wangu na kuinywa damu
 Hukaa kwangu nami hukaa ndani yake.
- Hicho chakula chenye uzima kweli ni mimi.
 Kilichoshuka toka mbinguni kwa Baba.
 Mtu akila chakula hiki hatafariki.
 Bali anao ule uzima wa milele.
- Kile chakula ninachotoa ni mwili wangu,
 Kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.
 Msipokula huu mwili wake mwana Adamu.
 Hamna 'zima ndani yenu.
- Anayekula huu mwili wangu na kuinywa damu
 Ana uzima, nami nitamfufua.
 Na mwili wangu ndicho chakula kile cha kweli.
 Na damu yangu ndicho kinywaji cha kweli
- Na kama Baba aliye hai 'livyonituma,
 Nami ni hai, ndimi hai kwa Babangu.
 Na kadhalika, mwenye kunila ana uhai,
 Kweli nasema atakuwa hai kwangu,