Cha Kutumaini Sina

Cha Kutumaini Sina
Performed bySauti Tamu Melodies
AlbumNyimbo za Sifa
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerEdward Mote
VideoWatch on YouTube
Views221,218

Cha Kutumaini Sina Lyrics

  1. Cha kutumaini sina, ila damu yake Bwana
    Sina wema wa kutosha, dhambi zangu kuziosha

    Kwake Yesu nasimama, ndiye Mwamba ni salama
    Ndiye Mwamba ni salama, ndiye Mwamba ni salama

  2. Damu yake na sadaka, nategemea daima
    Yote chini yakiisha, Mwokozi atanitosha.
  3. Njia yangu iwe ndefu, Yeye hunipa wokovu
    Mawimbi yakinipiga, nguvu zake ndiyo nanga
  4. Nikiitwa hukumuni, rohoni nina amani
    Nikivikwa haki yake, sina hofu mbele yake