- Cha kutumaini sina, ila damu yake Bwana
Sina wema wa kutosha, dhambi zangu kuzioshaKwake Yesu nasimama, ndiye Mwamba ni salama
Ndiye Mwamba ni salama, ndiye Mwamba ni salama
- Damu yake na sadaka, nategemea daima
Yote chini yakiisha, Mwokozi atanitosha.
- Njia yangu iwe ndefu, Yeye hunipa wokovu
Mawimbi yakinipiga, nguvu zake ndiyo nanga
- Nikiitwa hukumuni, rohoni nina amani
Nikivikwa haki yake, sina hofu mbele yake
|
The Solid Rock
|
|