Mimi ni Mkate wa Uzima
Mimi ni Mkate wa Uzima Lyrics
- Mimi ni mkate wa uzima, ajaye kwangu hataona njaa.
Mtu hawezi kunijia kamwe, asipovutwa na Baba yangu.
Nitamfufua kweli, nitamfufua kweli
Nitamfufua kweli, siku ya mwisho.
- Mkate huu ni mwili wangu, kwa uzima wa ulimwengu.
Aulaye mkate huo, kweli ataishi milele yote.
- Mimi ni ufufuko, Mimi ni uzima,
Yeye aniaminiye ajapokufa, atakua hai.
- Mimi ni njia, mimi ni mlango,
Aingiaye kwa mimi, ataokoka na kushibishwa.
- Ee Bwana, twaamini, wewe ndiwe yule
Mtakatifu wa Mungu, ulituletea kweli uzima.