Mwamba Wenye Imara
Mwamba Wenye Imara | |
---|---|
Performed by | - |
Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
Views | 57,075 |
Mwamba Wenye Imara Lyrics
- Mwamba wenye imara, kwako nitajificha
Maji hayo na damu, yaliyo toka humu
Hunisafi na dhambi, hunifanya mshindi - Kwa kazi zote pia, sitimizi sheria
Nijapofanya bidii, nikilia na kuudhi
Hayaishi makosa, niwe wa kuokoa - Sina cha mkononi, naja msalabani
Nilitupu, nifike, ni mnyonge, nishike
Nilimchafu naja, nioshe nisijafa - Nikungojapo chini, na kwenda kaburini,
Nipaapo mbinguni, na kukwona enzini
Roho yangu naiwe, rahani mwako wewe