Mwana wa Mungu
| Mwana wa Mungu | |
|---|---|
| Performed by | - | 
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) | 
| Views | 10,012 | 
Mwana wa Mungu Lyrics
- Mwana wa Mungu, Yesu Kristu,
 Bwana ninakuomba unisikie.
 Mimi mdhambi ninatubu.
 Bwana unisafishe na damu yako. *2{ Bwana unisafishe, hakika sina wema
 (sina wema) bila neema yako,
 Mimi mwenyewe sina uwezo } *2
- Nina imani kwako Bwana,
 vile ulinifia msalabani.
 Ulichukua dhambi zangu,
 Ukanifungulia kwako mbinguni *2
- Mungu wa amani na mapendo,
 Mimi nitatukuza jina lako kuu
 Unishike mkononi,
 kazi yake shetani kutupoteza *2
- Na kazi yangu ikiisha, Bwana,
 Ninatamani kuja kwako juu,
 Niwe pamoja na wateule,
 Tukitumikia mpaka milele. *2
 
  
         
                            