Mwana wa Mungu Lyrics

MWANA WA MUNGU

 1. Mwana wa Mungu, Yesu Kristu,
  Bwana ninakuomba unisikie.
  Mimi mdhambi ninatubu.
  Bwana unisafishe na damu yako. *2

  { Bwana unisafishe, hakika sina wema
  (sina wema) bila neema yako,
  Mimi mwenyewe sina uwezo } *2

 2. Nina imani kwako Bwana,
  vile ulinifia msalabani.
  Ulichukua dhambi zangu,
  Ukanifungulia kwako mbinguni *2
 3. Mungu wa amani na mapendo,
  Mimi nitatukuza jina lako kuu
  Unishike mkononi,
  kazi yake shetani kutupoteza *2
 4. Na kazi yangu ikiisha, Bwana,
  Ninatamani kuja kwako juu,
  Niwe pamoja na wateule,
  Tukitumikia mpaka milele. *2
Mwana wa Mungu
CATEGORYKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
 • Comments