Ninakuabudu Mungu Wangu
Ninakuabudu Mungu Wangu | |
---|---|
Performed by | St. Joseph Cathedral Dar-es-Salaam |
Category | Ekaristia (Eucharist) |
Composer | Joseph Makoye |
Views | 20,788 |
Ninakuabudu Mungu Wangu Lyrics
- Ninakuabudu Mungu wangu,
Unayejificha altareni,
Ninakutolea moyo wangu,
Usiofahamu siri yako. - Mafahamu yangu yadanganya,
Yanapokuona na kugusa,
Namsadiki Yesu hadanganyi,
Yeye Mungu Mwana na ukweli - Waficha Umungu msalabani,
Na ubinadamu altareni,
Nami naungama zote mbili,
Kama mwivi yule mwenye toba. - Thomas aligusa majeraha,
Nami nasadiki bila shaka
Ewe Yesu nipe pendo lako,
Tumaini kwako na imani - Umeteswa nini Bwana mwema,
Kwa kunipa mkate wa uzima
Yesu unifiche ndani yako,
Ili nilionje pendo lako - Yesu Pelikane nitazame,
Na kwa damu yako nitakase
Tone moja ndilo linatosha,
Na dunia yote yaokoka - Ndani ya mafumbo Yesu yumo,
Atafunguliwa kwangu lini?
Nikuone Yesu uso wako,
Nishiriki nawe heri yako. Amina.