Nipokee Bwana Nipokee
Nipokee Bwana Nipokee Lyrics
- Nipokee, Bwana wangu, nipokee,
Mbele zako nipo daima,
Sinitupe mbali nawe miye mdhambi,
Nipokee, Bwana wangu nipokee.
- Nakupenda Yesu mwema, nakupenda,
Kwa hiari yako U name,
Usinione kosa langu, nisamehe,
Nakupenda, Yesu mwema, nakupenda.
- Uje kwangu, Yesu mwema, uje kwangu,
Tumaini langu ni kwako,
Vya dunia hudanganya, huumiza,
Uje kwangu, Yesu mwema, uje kwangu.
- Siondoke, Yesu mwema, siondoke,
Nisiachiliwe gizani,
Kaa nami, moyo wangu wakutaka,
Siondoke, Yesu mwema, siondoke.
- Ninakupa mali yangu, ninakupa,
Ona ninakurudishia,
Nifundishe kutumia vyote kwako,
Ninakupa mali yangu, ninakupa.