Ukaristia ni Yesu
Ukaristia ni Yesu Lyrics
- Ukaristia ni Yesu sadaka,
Ukaristia ni Yesu chakula,
Ukaristia ni mwili wa Yesu.
- Ukaristia ni mkate wa Mungu,
Ukaristia ni mana ya kweli,
Ukaristia ni uzima wetu.
- Ukaristia ni damu ya Yesu,
Ukaristia ni kinywaji chetu.
Ukaristia ni chem chem ya neema.
- Yesu mwenyewe ametufundisha.
Yesu mwenyewe amefumbulia.
Neno la Mungu nani atakana?
- Sogea meza yake takatifu,
Kwa moyo safi nawe umpokee,
Atatolea nyingi zake neema
- Mungu mwamini, nakutumaini,
Ee Mungu mzima, ninakushukuru,
Ee Mungu wangu, nakupenda sana
- Sadiki, mkristu, upate wokovu
Ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu,
Mwisho mbinguni atakupokea