Asante Mungu Wangu
Asante Mungu Wangu Lyrics
Asante Mungu wangu asante,
moyo wangu wakusifu Aleluya.
- Natamani rukaruka kama ndege,
kwa furaha nifike huko mbinguni
Natamani kuwika kama jogoo,
Kuonyesha furaha niliyonayo
- Mungu wangu ni mkuu namtukuza,
hansinzii na halali sikieni
Ukilala yeye halali ni mlinzi wangu,
Na mchana sambasamba twatembea
- Hunilisha huninywesha siku zote,
Mungu wangu wa ajabu asifiwe
Posho langu sitaona njaa kamwe,
Maji yangu sitaona kiu kamwe
- Malaika juu mbinguni wanaimba,
wakisema hosanna atukuzwe
Wateule juu mbinguni wanaruka,
Wateule duniani tufanyeje