Bwana Anachunga
Bwana Anachunga |
---|
Performed by | - |
Category | Zaburi |
Composer | (traditional) |
Views | 4,922 |
Bwana Anachunga Lyrics
- Bwana anachunga uzima wangu,
Na malisho yake raha tele
Malisho mwake yale mabichi,
Kamwe mimi sitapungukiwa.
Bwana ndiye kweli mchungaji mwema
Sitahitaji kitu chochote
Penye majani yale mabichi, ndipo Bwana atanilisha.
Sitahitaji, kitu chochote kitu chochote sitahitaji
Penye majani yale mabichi yale mabichi penye majani.
- Penye maji mazuri matulivu,
Ndipo anaponiburudisha
Ananiongoza pasipo shaka
Njia nzuri, adili na nyofu.
- Mabondeni mwa uvuli wa mauti
Ninapopita sitaogopa
Kwa maana Bwana yupo na mimi
Gongo na fimbo vyako faraja.
- Meza waniandalia vitamu,
Nitashiba mbele ya watesi
Kichwa changu mafuta umepaka
Kikombe changu chajaa mema
- Wema na fadhili zote za Bwana
Zimenijia mpaka milele
Ninaomba kwake mchungaji wangu
Nikae kwake hata milele.